MWIGIZAJI na mwanamuziki wa muziki wa bongo fleva katika
staili ya Dance hall, Baby Madaha, amesema filamu mpya aliyoigizia Kenya The
Gal Gradder inatarajia kutoa 25 Desemba.
Akiongea na Bongo Unit, alisem filamu hiyo ambayo inamilikiwa na kampuni ya Candy n Candy, ameifanyia katika miji ya Nairobi na Mombasa
nchini Kenya, na sehemu chache za Tanzania.
Alisema
filamu hiyo itakuwa nzuri, kwakuwa waliofanya filamu hiyo si wababaishaji
wanachojali ni ubora wa kazi na sio ilimradi ikamilike.
“Filamu
imekusanya watu wa kila aina tumeingia mitaani, na kila sehemu si unajua Candy
n Candy wapo kikazi zaidi,” Alisema.

No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi