
NYOTA wa filamu nchini Haji Adam, amesema
atahakikisha elimu yake anasaidia sanaa ya filamu kufika mbali kwa kiwango kile
kinachotakiwa.
Akizungumza
wakati akiingoza filamu ya Wekeza Inalipa, mhitimu huyo wa chuo cha sanaa Bagamoyo ‘TASUBA’
alisema, sasa sanaa imetanuka ni vizuri zaidi wasanii wakaisomea.
Alisema
kwasasa amemaliza elimu ya stashada ya sanaa ya
uigizaji, lakini analego la kuongeza elimu zaidi ili kuweza kuifanya
taaluma hiyo kwa kiwango cha juu.
Aidha
alisema kama wasanii au waongozaji wa filamu, kama watakuwa wakiongezia na
elimu taaluma waliyonayo itakuwa ya kiwango cha juu zaidi.
“Kipaji
ukiongezea na shule basi unafanya kazi iliyobora, na kila mtu ataipenda kazi
yako” alisema.
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi