Watu saba
wamekufa papo hapo na wengine 21 kujeruhiwa vibaya katika eneo la
Chang’ombe, Barabara ya Segera – Chalinze, wilayani Korogwe, Tanga baada
ya mabasi mawili madogo ya abiria waliyokuwa wakisafiri kugongana uso
kwa uso.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe alisema jana kwamba
ajali hiyo ilitokea juzi saa 10:20 jioni baada ya gari moja kukwepa
mbuzi waliokuwa wameingia barabarani.
Alisema majeruhi wamelazwa katika Hospitali ya Magunga.
Alisema kati ya waliofariki, watatu walitambulika majina yao akiwemo
dereva wa moja ya mabasi hayo aliyefahamika kwa jina moja la Kombo.
Wengine ni mkazi wa Muheza, Martin Simon (35) na mkazi wa Korogwe, Juma
Abdallah (37).
Aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni Valerian Richard (27), Mohamed Juma
(60), Halima Abbas (35), Ali Rashid (61), Asha Bakari (39), Rehema
Hassan (39), Ibrahim Ramadhan (26), Omari Issa (30), Issa Ibrahim (30)
na Shaaban Hamza(35)
Wengine ni Ramadhan Mdangula (30), Mwanahawa Selemani (25), Mariam
Ramadhan (24), Theresia Gabriel (35), George Ernest (25), Issa Mohamed
(32), Fatma Hassan (48), Sharifa Bano (40), Shida Bano (27), Abel Elia
(35), Fadhil Rajabu (28) na mwingine aliyefahamika kwa jina moja la
Marijani.
Kamanda Massawe alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa ajali hiyo ilisababishwa na mwendo kasi wa mabasi yote mawili.
Akizungumzia matukio ya ajali na kuelekea mwisho wa mwaka, Kamanda
Massawe aliwataka madereva kufuata sheria za usalama barabarani ikiwa ni
pamoja na kuacha kuendesha magari kwa kasi.
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi