HUENDA
usishaagae kuona wasanii wengi wa filamu kuona wakimiliki magari ya thamani,
huku ukijiuliza kwa filamu gani walizocheza mpaka kumiliki magari hayo.
Lakini
kikubwa unaweza kujiuliza kwanini wasanii wanaomiliki magari hayo ni wanawake
na wanaume wamekuwa wakiangaika, na kulalamika kwamba maisha ni magumu.
Lakini kwa
msanii mwenye mvuto wa aina yake na kipaji cha kipekee, Irene Poul, yeye
amekuwa tofauti sana, kuhusiana na maslahi makubwa ya wasanii wenzake kwa kazi
ndogo wanazofanya.
Akizungumza
na mwandishi wa makala hii, Irene anaelezea zaidi kwa jinsi wasanii wengi wa
kike wanavyojikuta wakishindwa kuendesha kampuni zao za filamu kutokana na
vikwazo wanavyokutana navyo.
Anasema
alipoingia kwenye tasnia hiyo, aliamua kufanya iwe kazi hivyo alijikuta akifanya kazi nyingi bule
kwakuwa alikuwa akitafu ta jina na umaarufu.
“Nilikuwa
najua nini nakifanya, hivyo nikawa nafanya kazi nyingi za watu bule bila ya
malipo” anaelezea.
Kwakuwa
alikuwa akiigiza filamu za watu anasema alianza kutumikishwa, kama kulazimisha
kumkisi mtu na hata kuonyesha vitu vya kimapenzi, ingawa kwake alikuwa akiona
zipo njia nyingine kwa kuonyesha hisia za wapenzi bila kupeana kisi.
Vitendo
hivyo anasema vilianza kumfanya kutamani kuigiza filamu zake, ambazo atatumia
hisia za kimapenzi zaidi kuliko vitendo.
Anasema
kwakuwa alikuwa hana uwezo, hivyo ilimlazimu kuendelea kutumikishwa.
Lakini
anasema hapo ndipo wasanii wengi, wanajikuta wakikata tamaa na hata kutumishwa
biashara zingine kwa kuwa wameingia kwenye tasnia wakiwa na malengo mengine.
“Ujue wasichana
wengi wanaoingia kwenye tasnia ya filamu, wanakuwa hawajitambui na ndiyo maana
wamekuwa wakishindwa kuendelea,” Anasisitiza.
Irene
anasema mara nyingi , alijikuta akifikiria zaidi maisha yake ya baadaye hasa
kwa wale wanaojifunza kupitia yeye.
Anasema pia
alikuwa akijiuliza ni jinsi gani baadaye atakuja kumwangalia mwanaye, kama
akifanya vitu ambavyo baadaye vitamsuta katika jamii, kwa kuigiza filamu za
kuvaa ovyo, au kwenye biashara iliyonje ya sanaa.
“Niliweza
kukua kisanii ingawa kipato ambacho nlikuwa
nikipata kilikuwa hakikidhi mahitajii,” anaelezea zaidi.
Irene
anasema lakini baada ya kuhangaika kufanya kazi za watu ndipo alipojipanga
kufanya kazi zake mwenyewe.
Hapo ndipo
akajipanga na kufanya filamu yake ya kwanza aliyoipa jina la Kalunde.
Anasema
kufanya filamu hiyo kulimsumbua sana kutokana na uchanga wa kufanya filamu
zake.
Changamoto
alizozipata zilimchosha kiasi cha kufanya kitu kwa ubora ambao hakutarajia.
Anasema Lengo
lilikuwa kutoa filamu ambayo ilikuwa na kiwango cha juu, lakini alijikuta akishindwa
kukamilisha lengo hasa kutokana na bajeti.
Kutokana na
ufinyu wa bajeti, anasema kazi nyingi
kama kuwaendesha wasanii, kutafuta maeneo ya kuigizia ‘Location’, Production
Mananger zote alikuwa akizifanya
mwenyewe.
“Hapo ndipo nilipogundua ugumu wa kazi hii,
lakini nikajitahidi hivyo hivyo na kazi ikaisha,” anaendelea kuelezea msanii
huyo.
Anasema
lakini kubwa zaidi likaja juu ya kampuni ambayo alilipa fedha, kwaajili ya
kukamilisha production, ili kupewa
filamu yake.
Kwakuwa
alikuwa mgeni katika masuala ya kuigiza, anasema hakujua kama makampuni ya
‘Production’ huwa hayalipwi fedha zote kutokana na usumbufu wao.
Kwakuwa alimlipa
fedha zote, alijikuta akiingia kwenye usumbufu mkubwa kiasi cha kuchelewa kwa
filamu yake.
“Ujue
wanaume wanaweza kutumia nguvu, katika kukamilisha mambo yao na hata kumudu
purukushani, ili kazi yao iende upesi,” anasema.
Filamu hiyo
ilimsumbua kwakuwa wakongwe walimuona kama ni msanii mchanga, na kumchukulia
‘poa’, na kumdharau.
‘Kila mtu
alikuwa akinichukulia poa kiasi cha kujikuta nafanya kazi nyingi kwa wakati
mmoja jambo ambalo lilikuwa likinichosha sana” anasema.
Hata hivyo Irene
anasema amekuwa msanii mwenye bahati sana, kwakuwa anajiamini.
Kwa mara ya kwanza
kuingia kwenye tasnia, anasema ilikuwa mwaka 2010 ambapo alicheza filamu Morning Alarm.
Filamu hiyo
pia zilikuwa miongoni mwa filamu za
mwanzo kabisa za marehemu Steven Kanumba akiwa chini ya mwongozaji ‘Director’
Gabriel ‘Mtiti Game’.
Akiwa katika
filamu hiyo, aliweza kukutana na waigizaji wengine kama Ben Branco na Patcho Mwamba.
“Niliweza
kuwajibika vizuri kwa kuonyesha uwezo wangu kiasi cha kuanza kukubalika na watu
wengi” anasema
Kuonyesha
kwamba ni msanii wa kike ambaye amekuwa na bahati kubwa, yeye ndiye msanii wa
mwisho kuigiza na marehemu Steven Kanumba, na Hussein Mkiet ‘Sharomilionea’
katika filamu ya Love and Power.
Irene
anasema msanii ambaye amekuwa akimfuata nyayo zake kama kioo chake ‘Realy
Model’ ni mwigiza wa Hollywood, ni Angeline Jolie.
Anasema
zaidi ya kumpenda, lakini pia amefanana naye.
Filamu
ambazo alizowahi kuigiza ni nyingi sana lakini zikiwemo, Penzi la Kiza akiwa na Issa Mussa ‘Cloud 112’
na Dereva Bajaji akiwa na Salum Haji ‘Mboto’ ikiwa filamu ya vichekesho
maarufu kama mtindo wa ‘Romantic
Comedy’.
Kwa sasa
anasema anatarajia kutoa filamu yake ya pili ambayo itaitwa, Mjuto,
akishirikiana na Slim Omari, Mama Wele, na Salma Jabu ‘Nisha’.
“Hiyo ni filamu ambayo naandaa mwenye chini
kampuni yangu, ambayo itakuwa nafanya kazi zangu mwenyewe.” Anasema nyota huyo. Mafanikio
makubwa anasema aliyoyapata ni kuweza kumudu kuendesha kampuni yake ya Krema
Production, kuwa na usafiri wake na kuweza kumudu maisha yake kwa kutegemea
zaidi kazi ya filamu.
Mwisho
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi