Najua uwe mpenzi wa siasa, au si mpenzi wa Siasa, lakini kwa hili najua lazima utashituka kutokana na taarifa ya Chama cha Chadema juu ya kumvua Nyadhifa zote, Naibu Katibu mkuu wake
Zitto Kabwe ambae ni mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Mwanasheria
mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu kwenye makao makuu ya chama hicho, amesema Zitto na
wenzake watatu wamebainika kukihujumu chama kwa kuanzisha kitu kinaitwa
Mkakati 2013 kinacholenga kukisambaratisha chama hicho ili kuwaondoa madarakani
Mwenyekiti na Katibu mkuu wake.
Nyadhifa
alizovuliwa ni Unaibu katibu mkuu pamoja na Naibu kiongozi wa upinzani bungeni
ambapo yeye, Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba na mwingine mmoja Makao makuu
wamepewa siku kumi na nne wajieleze kimaandishi kabla ya kuchukuliwa hatua
zaidi za kinidhamu ikiwemo kuvuliwa Uanachama.
Lakini kikubwa bado watu wanajiuliza, nini kinafuata juu ya mwanaharakati huyu, aliyefanya vijana kupenda siasa? TUNANGOJE? Toa maoni yako kama unahisi unayo ya kutoa.

No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi