MNENGUAJI wa
kundi la Extra Bongo, Hassan Nyamwela ‘Super Nyamwela’ amekamilisha video ya
wimbo wake mpya wa Maneno, akimshirikisha Amini Mwinyimkuu ‘Amini’.
Nyamwela
alisema ameamua kubadilika kimuziki
kutoka katika uimbaji wa muziki wa dansi mpaka bongo fleva.
Alisema yeye
ni mwanamuziki hivyo kubalika kwake hakumuathiri kitu chochote huku akiamini
anaweza kufanya vizuri zaidi ya mwanzo.
“Mimi ni
mwanamuziki na naweza kuimba chochote katika muziki” alisema.
Super
Nyamwela alisema katika bendi ya Extra Bongo yupo kwa mkataba, hivyo haumzuii
kufanya kazi yoyote ya muziki.
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi