Kumekuwa
hakuna utamaduni wa utoaji wa tuzo kila mwaka katika tasnia ya filamu jambo
ambalo linadhorotesha ukuaji wa tasnia hiyo kwani watu wanakosa sehemu ya
kujipima kuhusu ubora wa kazi zao, kukosakana kwa tuzo ndani ya tasnia ya
filamu yenye miaka zaidi ya kumi na 13 ni aibu, tuzo hizi mara nyingi
ukwamishwa na taasisi ambazo zaidi ya kukusanya fedha hawajawahi kuandaa.
Pamoja na
mikingamo isiyo na tija kutoka katika taasisi mbalimbali mtandao huu hauwezi
kushindwa kuwatunuku wale wanaostahili kutunikiwa tuzo zao kulingana kazi zao
kwani tunaamini kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeona, tumetambua uwepo wao na
kazi zao pia, tunawaunga mkono kwa BORA ZA 2012.
Watayarishaji
wa filamu ni wakati wenu wa kuwakilisha filamu zilizotoka mwaka 2012 na kuingia
sokoni kwa ajili ya kupigiwa kura na wapenzi wenu wa filamu pia kwa wale
wasanii chipukizi wakilisheni kazi zenu mlizoshiriki na kuingia sokoni kwa
mwaka 2012.
Bora za
2012 zitawaleta washindi kwa utaratibu wa kupiga kura kupitia mtandao huu ,
kutuma ujumbe mfupi, wahusika ni wale wapenzi wa filamu Swahiliwood ambao
utembelea katika mitandao mbalimbali na vyombo vya habari kwa ujumla, tutakuwa
na vipengere 10.
MAKUNDI YA
FILAMUCENTRAL BORA ZA 2012.
Msanii
chipukizi wa mwaka
Muigizaji
bora wa kike
Muigizaji
bora wa kiume
Mwandishi
bora wa Mswaada
Mchekeshaji
Bora
Mtayarishaji
bora wa filamu
Kampuni
bora ya utengenezaji filamu
Msambazaji
Bora
Muongozaji
Bora
Tuzo
Maalum
KWA HABARI ZAIDI TEMBELEA www.filamucentral.co.tz na mitandao
mingine.
Mratibu
Myovela Mfwaisa
+255754 578 730
DAR ES SALAAM TANZANIA.

No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi