Baada ya
mwanamuziki Seif Shambani ‘Matonya’ kuibiwa vitu vyake vya ndani, na baadaye
Steve Mangele ‘Steve Nyerere’ kuibiwa Power window ya gari lake aina ya Verrosa..
sasa
mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Ismail Thabiti ‘Suma lee’ ameibiwa gari
lake aina ya Land Cruiser T 504 BRF,
maeneo ya Coco Beach ambapo alikuwa ameliegesha.
Suma Lee aliongea na Bongo Unit, na kusema kwamba aliliegesha gari lake maeneo ya Coco
Beach, na baadaye kwenda kuzunguka kidogo maeneo hayo, lakini baadaye aliporudi gari
hilo hakuliona.
Alisema
baada ya hapo alimfuata mlizni aliyekuwa maeneo hayo,ambapo wakati anakuja kuliegesha alimuona, hivyo akaanza kumuuliza jambo ambalo lilimpelekea kushikwa na hasira na kupishana naye maneno.
Alizidi kufunguka na kusema kwamba baada ya hapo, akaja muhusika wa hapo na kumchukua na kumpeleka kwenye kituo cha polisi cha Ostabai.
“Lakini
polisi sikukaa nikatoka na kufungua Rb katika kituo cha hapo hapo Ostabei
Polisi” alisema.
Alisema
namba aliyofungulia ni OB/RB/19237/2012, ambayo itamwezesha kumtafuta mtuhumiwa
wake popote na kumfungulia mashitaka.

No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi