Baada Ya
kujitoa kwa Msanii Suma Mnazaleti na meneja Maneno, kundi la burudani ya muziki wa kizazi kipya la
‘Mtanashati’ siku ya jumamosi linatarajia kufanya uzinduzi
wake mpya katika Ukumbi wa Club Billicanas, uliopo katikati ya Jiji la
Dar es salaam, eneo la Posta..... (Bonyesha Read More)
Akizungumzia
uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa
‘Mtanashati Entertainment’ Ostaz Juma na musoma, alisema tayari
maandalizi ya uzinduzi huo yamekamila na kuongeza kuwa kinachosubiriwa ni muda
ili kuwadhihirishia kile kilichokusudiwa.
Alisema
katika uzinduzi huo utakaotumika pia kwa ajili ya kuwatambulisha upya wasanii
wote watano wanaounda kundi hilo wakati huu ambao wanaendelea kujihimarisha
kimuziki ambapo pia amewaomba wapenzi wa burudani kujitokeza kwa wingi
kushuhudia uzinduzi huo.
Alisema
katika kupamba siku hiyo, ukiacha burudani kutoka kwa wasanii hao, pia
kutashushwa disco la nguvu hadi
kunapokucha na maarufu ‘DJ Ibra’ huku akisisitiza kuwa ‘usiku wa leo utakuwa moto wa kuotea mbali’.
“Baada ya
Mtanashati kuporomosha burudani wiki iliyopita katika ukumbi wa Maisha Club,
wiki hii kazi inahamia Billicanas’ bila shaka watu wote walioudhuria burudani
ya pale Maisha wanakumbukumbu nzuri juu ya burudani ya nguvu iliyofanywa na
Dogo Janja na PNC, burudani ya leo ni zaidi ya ile ya Maisha” alisisitiza Ostaz
Juma na musoma.
Alisema
katika uzinduzi huo, kundi hilo litapiga nyimbo mbalimbali zikiwemo mpya pamoja
na zile zinazoendelea kutamba katika vituo mbalimbali vya redio na
televisheni 'Ya Moyoni' 'Checherumba' ‘watasubiri’ na zinginezo zikitarajiwa kutumbuizwa
katika uzinduzi huo.
Mtanashati
ni kundi linaloundwa na wasanii watano ambao ni Dogo
Janja, Amazon, Y-Fil, PNC, Happy Balice ndani ya familia ya ‘Moja ya Muziki’
iliyopewa jina la ‘MTANASHATI ENTERTAINMENT’ chini ya Mkurugenzi wake Mkuu
‘Ostaz Juma na musoma’ ambaye kwa mujibu wake malengo makubwa ya
kuanzishwa ‘Mtanashati’ kumekusudia
mapinduzi mapya katika tasnia ya
Muziki wa Kizazi kipya
Ends.

No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi