Wednesday, August 8, 2012

Nyumbani Lounge yafungwa


Wakati mumewe akijiandaa kurudi tena kwenye stesheni ya redio mwanamuziki Lady Jay Dee, anayemiliki mgahawa maarufu hapa jijini Dar es salaam unaojulikana kama Nyumbani Lounge, ameamua kuufunga Mgahawa huo. Meneja wa mwanamuziki huyo na mume wa mwanamuziki huyo, amesema kufungwa kwa mgahawa huo ni kuweza kuufanyia marekebisho, kwa upande wa ndani na nje wa Mgahawa. Pia amesema zaidi ya kufunga kwaajili ya marekebisho pia, wamefanya mapumziko kwaajili ya mwezi mtukufu wa ramadhani, kwani wanatarajia kuufungua tena katika sikukuu ya Idd. 
Nyumba Lounge

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi