Mwanamuziki ambaye amejipatia umaarufu mkubwa katika kundi la Kikosi cha Mizingi, Kalapina ameshakamilisha wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Harakati akishirikiana na Stive Artisi anayeishi Marekani. Kalapina amesema katika wimbo huo ameeleza maafa mbalimbali yanayoikumba Tanzania kutokana na wimbi la mafisadi. Aidha alisema pia wimbo huo umelezea maisha ya Dr Ulimboka, ambaye alipata kipigo cha kung'olewa meno na kucha na watu wasi julikana,na kusema kwamba mambo hayo yote ameyatengenezea filamu.
 |
| Karapina amesema maisha yote ya Ulimboka, alienda kuyachunguza na kuyafanyai filamu moja, ambayo yeye ndiye atakayeigiza kamaDr Ulimboka. |
 |
| Mwisho alimalizia kwa kusema wimbo wa Harakati, ndiyoutakuwa Soundtrack ya filamu hiyo. |
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi