Tuesday, August 7, 2012

Captain G Habash kurudi tena radioni

Mtangazaji mahili ambaye alifanya vizuri sana katika kipindi cha Jahazi ambacho sasa kinarushwa na Anord Kayanda, Kibonde na Wasiwasi katika stesheni ya Cloud Fm muda wa jioni, na baadaye kuachana na kazi hiyo na kujitosa katika kuhudumia mgahawa wake wa Nyumbani Lodge akiwa na mkewe mpendwa ambaye ni mwanamuziki Lady Jay Dee, Captain Gadner G Habash anatarajia kurudi tena katika utangazaji.  Captain G. Habash alisema kwamba safari yake hiyo itaanza mwezi wa 9, lakini hakusema ni kipindi gani hataendesha wala hakusema kwamba ni redio gani, lakini amewaambia mashabiki wake na wapenzi wake wanaopenda kumsikia tena hewani basi anakuja kwa hewa hivi karibu. Muda kipindi na redio anayotaka kuitangazia vyote utavipata kuvisikia hapahapa Bongo Unit, naomba usikose ku LIKE, page hii na kuingia kila siku Bongo Unit ili kujua mengi yanayowahusu watu maarufu.

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi