Mmiliki wa bendi ya Twanga Pepeta Asha Baraka, amekana kwamba hakuongea lolote na gazeti lolote kuhusiana na bendi yake ya Twanga Pepeta la kuhusiana na jinsi inavyoendelea na ratiba yake katika mwezi huu mtukufu wa ramadhani Kareem. Asha alisema hataki kugombanishwa na dini yake, na magazeti kwakuwa yeye ni muislam kamili. Aidha amesema yanayoandikwa kwenye magazeti hayo, yeye wala hausiki na hajawahi kuongea, kwani anaamini atakapoongelea suala hilo atakuwa anakiuka maadili. Mwisho amedai kwamba hayo yote atakuja kuongelea baada ya mfungo wa Ramadhani Kareem huu kuisha.

No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi