Thursday, August 16, 2012

Anayemnyima Afande Sele Usingizi ni huyu..

Pindi ukimpigia simu Mfalme Seleman Msind 'Afande Sele', na akapokea kama atakujua kama wewe mwandishi au swahiba wake wa karibu Stori ya kwanza kukupa ni hii. Kwamba hadi sasa anamlalamikia rafiki yake wa karibu na aliyempa nuru kwenye muziki MHESHIMIWA JOSEPH MBILINYI  maarufu kama Mr Two au Sugu kwa kutomfanyia mpango wowote, juu ya maslahi yake ambayo aliyafanya juu ya mikakati ya  Maralia kwa madai kwamba mpango ule hakuwa wa peke yake ila na yeye yumo. Afande analonga zaidi kwamba hata katika wimbo wa Maralia ambao wasanii nane wanautumia katika harakati za kupambana na ugonjwa huo, yeye hayupo wakati ndiye aliyeutunga na kuumba. Afande anazidi kulia na Sugu kwamba hata ule mpango aliujenga naye kwaajili ya kuingia Bungeni  kutetea haki za wasanii haupo tena ila anakwenda kwaajili ya maslahi yake. Hakuishia hapo zaidi na zaidi Afande alilalamika jinsi Mheshimiwa Sugu, anavyogomakuipokea simu yake,  kila anapojaribu kumpigia mkuu huyo wa Ant Virus hapokei  simu yake jambo ambalo linamzidishia  hasira. Anasema hivi sasa ameamua kujipanga mwenyewe na aende mjengoni kwaajili ya kufanya kazi mwenyewe za kutetea HAKI za wasanii wa Tanzania. Yaani kila anapolala anawaza Bungeni na watu ambao aliamini wangefanya kazi, hakufanya tena. hivi sasa anamtoto wa Pili, baada ya Tunda ... Hilo ndilolinalomnyima Afande Sele raha.
Mhesimiwa Mbilinyi 'Sugu'

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi