usaili
wa Epiq Bongo Star Search unaoendelea Mwanza katika uwanja wa CCM
Kirumba. Ikiletwa kwenu kwa ushirikiano wa kampuni yako ya hapa hapa
Tanzania –Zantel. Mwamko wa washiriki umekuwa mzuri kuzidi mikoa mingine
yote tuliopita msimu huu. Kwani mpaka mwisho wa siku jana jumla ya
washiriki 480 walikuwa tayari wameshasajiliwa na bado usaili unaendelea
siku ya leo. Pia katika eneo la usaili tuko na watu wa damu salama
wakihamasisha watu kuchangia damu na mwamko wa washiriki umekuwa mzuri.
Majaji wameshafika eneo la usaili na usaili umeshaanza. Pamoja na
usaili, Zantel ilipata nafasi ya kukutana na madiwani wa mkoa wa Mwanza
na kuwagawa jumla ya simu za mkononi 50 zilizounganishwa na mtandao wa
Zantel chini ya kifurushi cha CUG (Closed User Group) ambao utawawezesha
kuongea bure kati yao. Mawazo
na michango yenu yanahitajika katika kuendeleza uhusiano mzuri na
katika kupata taarifa/picha bora zaidi. Kama utapenda tuongeze anuani ya
barua pepe ili kupata taarifa zitakazo kuwa zinatumwa, tafadhali ongeza
anuani hiyo na ujibu barua pepe hii ukiweka majina na wadau wengine wa
habari.
|
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi