Saturday, July 28, 2012

Masanja alipofutwa machozi na Bongo Movie

Mwigizaji wa kundi la Ze Comedy linalorusha vipindi vyake  katika kituo cha televisheni cha TBC, Masanja Mkandamizaji hapamajuzi kati alitolewa kimasomaso na wasanii wa Bongo Movie, wakati wa uzinduzi wa albamu yake ya kumsifu mungu ya, HAKUNA JIPYA, ambayo alienda kuinzidulia mkoani IRINGA. Kitu ambacho cha ajabu ambacho hakikutegemewa na wengi, kwamba katika usinduzi huo, hakukuwa na msanii hata mmoja ambaye anatoka katika kundi lake la  ZE COMEDY. Hakuwawa na Joti, Vengu, Mpoki, Kipara Makurega, baba Andunje  wala Seki ambaye kiongozi wa kundi hilo.(Mgeni rasmi Mheshimiwa Philp Mulugo Naibu Waziri wa elimu na mafunzo akizindua albamu hiyo, juu kwenye picha)


Lakini jambo la kutia Moyo katika tamasha lake lililoudhuliwa na wasanii kibao kutoka BONGO MOVIE, jambo ambalo linashiria kama vile wamekuja kumpa Support ambayo wenzake wamemnyima, na kuonyesha kwamba hayupo peke yake katika harakati zake za kumtafuta Mungu, kupitia nyimbo za Injiri pia na sanaa yake ya uchekeshaji.


(Richie rich na Maliam Ismail) Maswalimengi watu wanajiuliza, inamaana wote walikuwa bize kwenye kazi zao kiasi cha kutotokea hata mmoja, au kulikuwa na nini nyuma ya panzia.


(Stive Nyerere na  Baturi)


J B na Masanja


Kazi ilifanywa vizuri jukwaani na wasanii wote lakini Chopa Wa Mchopanga, alikamua vizuri na Mr Kupa






Mwisho wa Siku Masanja hakuamini macho yake kwamba alifunika vibaya, Hapa ndipo linapokuja swali Je!! Na wengine ambao wanaimba wakizindua albamu zao itakuwa hivi hivi?

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi