Monday, July 9, 2012

Zantel yazidi kuinogesha EBSS Arusha, yatoa simu kwa madiwani wake, vijana wengi wajitokeza katika usaili

Katika usaili uliofanyika,zaidi ya washiriki 750 walikutana na majaji na watu wasiopungua 1800 walijitokeza eneo la usaili. Majaji waliweza kutoa maoni yao juu ya vipaji vilivyojitokeza na kuhakikisha waliochaguliwa watakwenda kuwakilisha vyema mkoa wa Arusha. Katika matukio ya kijamii,  Zantel imetoa simu za mkononi 25 kwa manispaa ya jiji la Arusha ili kuwarahisishia mawasiliano viongozi na watumishi wa manispaa.Simu hizo ambazo zitasambazwa kwa Msitahiki Meya, Madiwani na mkurugenzi wa mji, zitawarusu kupiga simu bure wakati wote kwa kutumia huduma ya kipekee ya Zantel ya ‘CLOSED USER GROUP’.Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkurugenzi wa masoko wa Zantel, Bwana Deepak Gupta, alisema kampuni yake ina mkakati madhubuti wa kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kusukuma gurudumu la maendeleo. ‘Kwa simu hizi ambazo zina laini ya Zantel, watumishi wa manispaa wanaweza kuwasiliana bure kabisa baina yao hivyo kurahisisha mawasiliano na ushirikiano kwa vitengo mbambali vya manispaa pamoja na kupunguza gharama’ alisisitiza Bwana Gupta.
Usaili unaendelea katika mikoa mingine ambapo wiki ijayo usaili utafanyika mkoani Mwanza tarehe 14 na 15 za mwezi huu wa Agosti  Mawazo na michango yenu yanahitajika katika kuendeleza uhusiano mzuri na katika kupata taarifa/picha bora zaidi. Kama utapenda tuongeze anuani ya barua pepe ili kupata taarifa zitakazo kuwa zinatumwa, tafadhali ongeza anuani hiyo na ujibu barua pepe hii ukiweka majina na wadua wengine wa habari.
 

Kijana huyu ni mmoja kati ya vijana wlaiojitokeza Arusha kushiriki katika usaili wa EBSS lakini hakupata nafasi hiyo

Huyu nae alivutia sana kwa kulipiga gitaa kiumakini lakini hata hivyo hakupata
Majaji walilazimika kusimama ili kuhakikisha kuwa wanapata vema alama za kila mshiriki wa EBSS Arusha
Mwana dada Amina S Maliam  alionesha umahiri mkubwa wa kuimba siku ya kwanza lakini hata hivyo siku ya mwsiho hakuweza kufanya vema na alijikuta akiangau kilio sana
Alilazimika baadae kumfuata MadamRita kuomba ushauri wa kazi yake hiyo na aliahidiwa kusaidiwa
Amina hapa akiwa na mwanaye nani ya Club Triple A - Arusha kwenye usaili wa Epiq Bongo Star Search 


No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi