African Stars Band 'Twanga Pepeta'
Ijumaa ya wiki hii tarehe 29-06-2012 itatoa burudani katika
kinyang'anyiro cha kumsaka Redds Miss Kanda ya Kati onyesho
litakalofanyika Mkoani Dodoma.
Onyesho
hilo linataraji kufanyika siku ya Ijumaa katika ukumbi wa Club
Kilimani. Shindano la Miss Kanda ya Kati ni majumuisho ya washindi
watatu walioshinda kutoka katika Mikoa ya Redds Miss Tabora, Redds Miss
Singida, Redds Miss Dodoma na Redds Miss Kigoma yaliyofanyika hapo
awali, Washindi watatu wa Redds Miss Kanda ya Kati wataungana na wenzao
kutoka katika kanda nyingine ili kushiriki Shindano la Redds Miss
Tanzania litakalofanyika hapo baadae mwaka huu.
Twanga
inataraji kutumia fursa hiyo ili kuitambulisha single yao iliyokamata
Jiji kwa sasa ya 'Shamba la Twanga' kwa wapenzi wake wa Dodoma pia
tunataraji kuwaalika Waheshimiwa Wabunge wanaohudhuria vikao vya Bunge
la Budget ili nao wapate fursa kusikia single ya Shamba la Twanga. Mgeni rasmi katika onesho hilo anataraji kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dk. Fenella Mukangara.
Twanga
Pepeta wanataraji kuondoka siku ya Ijumaa alfajiri mara baada ya
kumalizika kwa onyesho Club Maisha na watarejea jijini Dar es salaam
siku ya Jumamosi kuendelea kutoa burudani katika ukumbi wao nyumbani wa
Mango Garden au maarufu kama 'Twanga City'. Twanga
itapeleka kikosi chake chote kilichosheheni wanamuziki wake nyota
watakaoongozwa na Meneja wa Bendi Khamis Amigo na Kiongozi luizer Mbutu.
KHAMIS AMIGO
MENEJA TWANGA PEPETA.
|
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi