| Wasanii wawili kutoka maeneo ya Mabibo Mwisho waliotamba na ngoma kama Jonita wakimshirikisha Mr Blue,na wimbo wa Sungula na Fisi, Ramadhani Kalisela 'Pingu' na Deogratus Frade 'Desso ' wameungana tena, katika kutoa burudani kwa mashabiki wao. Wasanii hao wamesema walipotengena walikuwa wakijisikia vibaya sana pindi watu walipokuwa wakimuuliza Pungu yupo wapi Desso? au Desso yupo wapi Pingu sababu majina yao yamezoeleka kutamkwa pamoja. Wamesema kwa sasa kila mmoja ingawa yupo kwenye kundi lake Desso yupo Tit Top Connection, lakini wanapokuwa pamoja watakuwa wanaunda kundi la Tatanisha Enter 'Gollira Killer', na wanajipanga kutoka na wimbo mpya wa Jicho usinibanie |
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi