| Tuzo za Kilimanjaro Music Award 2012, ambazo zilianza tour yake mapema baada ya kupatikana kwa washindi wa Tuzo hizo na kuanza safari ya kuwatangaza washindi hao pamoja na kutafuta vipaji vipya katika baadhi ya mikoa ya Tanzania bara. Tour hiyo imeifikia tamati katika viwanja vya Posta na Simu Kijitonyama siku ya jummosi. Wasanii mbalimbali walipanda jukwaani katika kutoa shukrani zao kwa Watanzania, ambao waliowapigia kura kwa mkoa wa Dar es salaam baada ya kufanya hivyo mikoani. Pia katika tamasha hilo ambalo ni kubwa wasanii walioshinda mikoani walipataa fulsa ya kupanda jukwaani pamoja na wasanii wakongwe, na baadhi ya wasanii walitoka mikoa ya Kigoma Arusha na Mwanza, pia waligewa nafasi ya kutengeneza nyimbo kutoka kwa Producer mkali mwaka 2012-2013 kupitia tuzo hizo Maneck wa Am Record. |
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi