Saturday, June 16, 2012

Baghidad kuwasha moto New Maisha Club

NYOTA  wa muzikiwa Bongo fleva  Godpray Kweka ‘Baghdad’  siku ya jumapili ya juni 17 mwaka huu  atazifungua kiu za mashabiki wake, baada ya kupotea kwa muda mrefu jukwaani pia atatambulisha kundi lake jipya la Wajukuu katika usiku wa leo Maisha Club.
Baghidad alisema  ingawa alikuwa kimya kwa muda wote huo, alikuwa akitafuta ni kitu gani afanye kwaajili ya mashabiki wake ambao siku zote wamekuwa naye pamoja.
Aliongeza kwa kusema tamasha hilo,litasindikizwa na Fidodido, Nurudin, Mabeste, Hemed Seleman ‘Phd’ pamoja na Chid Benzi.
“Nimejipanga kufanya ‘Surprise’ kwa kila mtu ambaye ataudhulia  tamasha hilo, kwakuwa ninamuda mrefu na nahitaji kufanya ambayo sikuwahi kuyafanya” alisema.


No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi