| Hakika katika kitu ambacho nimekuwa nikikiombea ni kuona hawa wakubwa zetu wakija na kitu kipya tangu kutengena kwao, Si dhani kama kuna mtu ni mpenzi wa muziki wa Bongo fleva, kisha hatamani kusikia tena sauti ya King Crazy Gk, akiwa na Ambwene Yesaya 'Ay' na Hamisi Mwijuma 'Mwana Fa'. Si dhamni!! Hii naamini hawa jamaaa ndiyo waliosababisha kuibuka kwa makundi mawili ya East Coast Team 'Watoto wa Upanga aka Mambo safi' na West Coast 'TMK watoto wa uswahili aka wazee wa mapanga' ambao kwa kiasi kikubwa wakachangia kukuwa kwa muziki wa kizazi kipya. Vijana na watangazi tulianza kujigawa kama Simba na Yanga, na kila aliyetaka kuimba alikuwa na kazi ya kwanza ni kuchagua awe mgumu kama kama Tmk au aimbe Komesho kama East Coast. |