| Mkali wa muziki wa Bongo Fleva Baghidad ambaye siku si nyingi alijiengua kutoka katika kundi la Mexicana Lacavera, amesema kwa sasa amestopisha utoaji wa nyimbo katika redio na hatmaye kugonga nyimbo zote katika Tv kwa mwaka huu wote hususani hii miezi mitano ya mwanzo. Baghidad alisema kufanya hivyo ni kutokana na kazi zake kujulikana sana na watu lakini kumjua hawamjui, jambo ambalo linapelekea kutojulikana na wengi hasa kupitia Tv. Msanii huyo ambaye ni mnene kuliko wasanii wote ambao wanavuma kwa sasa, alisema kwamba huenda akasikika katika redio kupitia nyimbo za watu za kushirikishwa, pia atakubali kushirikishwa na mtu ambao kazi zao watazisambaza, na sio kuziweka ndani kama urembo. Aliongeza kwa kusema kufanya hivyo vyote ili apate kujulikana zaidi kwa wadau wanaotizama kwenye Tv, kwakuwa Tv imekuwa ikimtambulisha mtu zaidi kuliko hata redio |
|