Sunday, April 29, 2012

Mr Nice kupanda jukwaani tena baada ya miaka sita kupita

Mwanamuziki ambaye alitamba sana na nyimbo kama Kikulacho, Fagilia na nyingine nyingi Lucas Mkenda 'Mr Nice' amepanga kuzindua albamu yake mpya itakayokwenda kwa jina la Tabia Gani. Mr Nice amedai kwamba zaidi ya miaka sita hajapanda jukwaani, hivyo kupanda kwake kwa safari hii, anatarajiakufanya vitu ambavyo alishawahi kufanya kwa mara ya kwanza na zaidi ya pale. Aidha alisema kwamba uzinduzi huo anatarajia kusindikizwa na wasanii kibao akiwemo Chege na Temba pamoja na Robart Mangwer 'Ngwer' katika Club Bilicanas siku ya tarehe 6. amesema show yake imedhamini na Samaki samaki, Epiq Nation na madukala Steal Soul.