Sunday, April 15, 2012

Mitindo ya mavazi ilivyoshika Kili Music Award

Katika tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards, watu walivaa katikamtindo tofauti, kila mmoja alivaa kwa kileambacho anahisi kwake ndicho alichokuwa akikifikiria kuvaa. Watu walipenda, na wabunifu pia walijitahidi kuonyesha ubunifu wao, hebu pata picha hizi tofauti............
Abdul Kiba, akiwa kwenye pozi na mrembo
Mama Asha Baraka, mkurugenzi wa ASET Enter wamilikiwa wa Twanga Pepeta.
Msanii chipukizi wa muziki wa bongo fleva, Betrice aka Nabisha naye alitoka kwa mtindo wa kipeke.
Bibi Cheka hakuwa nyuma, naye alisogea hadi Redcapert
Mwanamuziki wa Mashujaa bendi  Chaz Baba aka Kingunge, yeye alivua kabisa koti ili kuchambua kila kimoja kwa kile alichokivaa.
Mtangazaji wa Clouds Tv wa kipindi cha Ongea na Janeti, Janert akimuoji mtangazaji wa Clouds Fm Dina marious
Captain G Habas meneja na mume wa mwanamuziki Lady Jay Dee, akimchukulia mumewe tuzo, yeye alipiga penzi chini simple juu akamalizia na kotila suti.
mwanamuziki kutoka pande za Mwanza H. Baba yeye hakutaka kuangaikana suti, ila alivaa nguo ya damu ya mzee aina ya railoni, unyororo mfukoni, rozali na miwani meupe akawa amemaliza
Disner Martin na ndiye inasemekana ni meneja wa mwigizaji wa Movie nchini, Wema Sepetu, akiwa na mwanadada mtangazaji wa Clouds Tv Hellen Kazimoto.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Izzo B akijiweka sawa kidogo, yeye alipiga suti ya rangi kama unavyoiona.
mwanamuziki Jay Moe, alivaa suti nyeusi na kiatu cheusi.





Sureshi kutoka studio ya Mkubwa na Wanaye , Poteza Record iliyopo Temeke, naye alitinga na jeans.


Mfalme mzee Yusuph naye alikuwepo hapo na suti na juu akatinga na kofia ya Bongo man.
Kweli mkubwa ni mkubwa, alikuja na koti la gharama anaitwa Said Fella

Mtangazaji wa Clouds Media, Shadee, yeye akagonga bonge la mpasua wa fundi amejisahau
Jaffary mume wa Khadija Kopa, alipiga suti yake ya mchele mchele