| Msanii maarufu wa filamu nchini Issa
Mussa 'Cloud 112' amelazwa katika hospitali ya Al Ijumaa iliyopo Kariakoo baada ya kuugua
ghafra, wakati akiwa katika shughuli zake za kawaida. Cloud 112 amelazwa hospitalini hapo tangu saa saba mchana,na hivi sasa tayari ameshapata vipimo
vya Malaria ambayo amekutwa hana, pia akapimwa na presha ambapo alikutwa ipo
sawa, hali iliyopelekea kuchukua vipimo vya typhod. Hadi hivi sasa msanii huyo bado yupo
hospitali kwaajili ya kuendelea kuangalia afya yake na kuchukuliwa vipimo
zaidi, wakati huo pumzi ndiyo inayomsumbua kwa kuwa anaipata kwa tabu. |