| Baada ya mwanadada Rihana kuwakimbiza kwenye muziki na kufanya vizuri zaidi, ameamua kujiingiza kidogo kwenye filamu ili kuona na upepo wa huko unaendaje. Mwanamuziki huyo ambaye aliyewahi kuwa na uhusiano na Chris Brown na baadaye kupeana vipondo na kutengana, na sasa kulipotiwa kwamba wamerudiana kama mafriend, ameigiza filamu akiwa kama kamanda wa jeshi ambaye anajihusisha na siraha kali na za kisasa akitumia jina la Raikes. Ansema sio kwamba kuwa mwanajeshi ni kubahatisha, ila alishawahi kupitia jeshi wakati yupo kishule shule, jambo ambalo anaamini ndilo lililomfanya afanye vizuri kwenye movie hiyo. |
|
|