Saturday, March 17, 2012

Part ya Bongo Movie ya mwaka mmoja.

Wasanii kibao ambao wanaunda Bongo Movie jana walikuwa wakihadhimisha mwaka mmoja tangu kuundwa kwa kampuni hiyo, ambayo inajishughulisha na mambo kibao ikiwemo uigizaji pamoja na michezo kama mpira na basketball kwa wanawake. Kiongozi wa bendi hiyo Jacob Stephan, alieleza sababu mbalimbali ambazo zilipelekea tamasha hilo kukukamilika, huku akitaja uongozi mzima ambao unaunda Bongo Movie.
Sheeta 'Chif Mswati' akiwa kwenye pozi wakati ajivuta kuwapa sapoti wasanii wafilamu
Jamani Bongo Movie kuzuri, hawa wote ni wadau na wengine wasanii kwa bahati majina yao sijayajua lakini ilikuwa burudani kwenda mbele
Kimwana wa Manyewe mwaka 2001 wanamwita Sajenti, ambaye pia kwa sasa naye ni muigizaji mzuri katika Bongo Movi
Hk ambaye ni Mc wa ukumbi wa New Maisha Club, akiwa na Tito Charlos muigizaji wa filamu za kibabe
Ah!! Mwanadada Maya!!
Hatmani akiwa na mshika hazina wa Bongo Movie na muigizaji wa kwanza kumiliki magari mawili ya kifahari Vicenti Kigosi aka Ray
Wapi Ali Akida akiwa amevaa kapero, anasema tayari ameshamaliziana na Mashujaa kwa hiyo sasa ni hivi ni mwanamuziki halali kabisa wa Mashujaa
Stive nyerere akiwa kwenye kikoti chake
Vinywaji vilikuwa vya kumwaga
Fidforce kiongozi wa bendi ya mashujaa, akiimba jukwaani
Wema hapa alikuwa na Stive Nyere, cha ajabu kila Stive alipokuwa akimwangalia Wema basi alikuwa akicheka sijui nini alikuwa akifikiria.
Hee!! Alipoonekana Barnaba, waigizaji wa filamu wakaita Shemmm!! lakini haikuwa tatiozo Shilole alipopanda jukwaani alimuita. Ndipo Barnaba Boy alipokwenda na kujua bonge la shangweee.
Barafu akiwa na Libert
Mashujaa wakiwa jukwaani, Aisha Twiga na Milinda Nyeusi
Jadol Fidforce na Chaz Baba
Hii ndiyo kamati nzima ambayo inaongoza wasani wa Bongo Movie, lakini wakiwa chini ya Jb na Cloud112
Angekuwa mwanamme ninge mwita pedezee Mama Lolwa, lakini mwamke sijui anaitwaje. Ni mmoja wa watu muhimu sana katika Bongo Movie
Binti Mfupi na machachari katika Bongo Movie, anaitwa Mainda ambaye yeye ni Stive Nyerere wanunda kampuni ta The Power Nyerere
Maswahiba wawili walipokutana hapa, kati ya Jb na Ray
Jackline Wolper ndani ya pozi
Huu ulikuwa muda wa burudani, huwezi amini Stive Nyerere alivyofunika pindi alipoanza kuimba Ki kongo.
Mwisho wa picha hii, ni Mtoto wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Ridhiwan, akiwasha mshumaa kwaajili ya kusherekea sherehe hiyo ya kutimiza kwa mwaka mmoja wa Bongo Movi, naye ndiye alikuwa mgeni Rasmi.

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi