Monday, March 19, 2012

Msanii wa filamu nusura kufa

Mwigizaji maarufu wa filamu nchini, ambaye kwa sasa anatamba na filamu ya Big Brother Lawrence Anthon 'Makala'  jana amepotea chupu chupu kufa katika ajali ya gari iliyotokea kati ya Geita na Morogoro. Mwigizaji huyo alisema ajali hiyoimesababishwa na uzembe wa madereva kwa kutaka ku over take gari lingine, hali iliyopelekea kuingia mtaloni baada ya kutaka kugongana  uso kwa uso na Lory.




Amesema anashukuru mungu kwenye ajali hiyo hakuna alifariki,ila watu walijeruhiwa sana.



Makala amesema ajali hiyo kwake imemweka katika hali ngumu, kwani usiku anakosa usingizi pindi anapokumbuka kile kilichotokea. Hata hivyo msanii huyo amesema hali yake ikiwa sawa, anatarajia kuachia filamu yake mpya.

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi