Monday, March 5, 2012

Fasha Joshua amrithi Lilian Internat Twanga Pepeta

Mwanamuziki aliyekuwa Dubai  Fasha Joshua amerudi upya katika bendi yake ya Twanga Pepeta, ilikuziba nafasi  iliyoachwa na mwanadada ambaye alikuwa mnenguaji wa kundi hilo Lilian Internet, ambaye kwa sasa ameamua kuhamisha makazi yake hadi Mashujaa kwa kina Chaz Baba. Kiongozi wa kundi la Twanga amesema amepotea taarifa za kuhama kwa mnenguaji wake huyo, lakini kwao haikuzuru kwakuwa tayari wanaye mnenguaji mwingine ambaye alikuwa likizo Uarabuni. Uongozi wa Twanga wamesema mnenguaji wao ameanza kazi rasmi jumatano hii, hivyo taratibu kazi zake zitaanza kuwa wazi mbele ya mashabiki wake.