Wednesday, February 22, 2012

Lil Gheto amkana Timburo


Mwanamuziki na mtayarishaji wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la Off Side Trick, Said Amdani ‘Lil Gheto’, amesema hausiki za mwibia nyimbo msanii Timbulo.
Lil Gheto amesema kwamba msanii huyo alikuja na kumuomba amtengezee wimbo, ambapo alianza kumuelekeza ni jinsi gani wimbo huo unatakiwa uwe.
Anasema yeye kama Prodyuza, alianza kutengeneza midundo kama alivyoelekezwa mpaka pale, ambapo mwenye wimbo huo aliporidhika napo.
“Hata mimi alinificha suala la yeye kukopi nyimbo ya mtu, ila nashangaa kila mmoja anasema mimi ndiye niliyeiba na kumpa yeye” alisema.
Mwanamuziki inasadikiwa ameiba wimbo huo kutoka kwa msanii  X maleya na wimbo wa Tchokolo, na yeye kuugeuza na kuita Waleo wa Kesho.
  

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi