Monday, February 27, 2012

Jaffarai atangaza kujitoa tuzo za Kili Music Awards

Mwanamuziki aliyewahi kuvuma na track kali kama nipo Bize na nyingine nyingi, ametangaza  huenda akajitoa kwenye tuzo za Kili Music Award kutokana na ubabaishaji ambao yeye ameuona. Huenda pia atakapojitoa akawa miongoni mwa wasanii waliotangaza kutoshiriki kwenye tuzo hizo kama ilivyo kwa mwanamuziki Dully Syskes, Hata hivyo  waandaaji wa tuzo hizo wamesema wao malalamiko hayo ya kujitoa, huwa hawayaelewi mpaka mtu atakapoyawasiliasha kwa njia ya barua.