Thursday, February 23, 2012

Bob Junior njia panda

Mwanamuziki kutoka kundi la Sharobaro Rec, Raheema Rummy ‘Bob Junior’ amesema hadi sasa bado yupo njia panda juu ya video moja kati ya video zake tatu ya Ngombe, Singasinga na Nichumu.
Akizungumza na mwandishi wa safuu hii amesema kwamba wimbo wake wa Singa singa ameufanyia Ulaya, na zingine amezifanyia hapa lakini zote alihitaji zitoke kipindi hiki.
Amsema hali hiyo imemfanya aangalie sana upepo wa muziki kwa sasa ili ajue huenda anaweza hata kuziachia zote kwa wakati mmoja.