Wednesday, September 21, 2022

Naibu waziri ataka kiwanda kurekebishe mfumo wa maji taka


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis ameelekeza kiwanda cha nguo cha A to Z kilichpomkoani Arusha kikamilishe ujenzi wa mtambo wa kutibu maji taka ndani ya miezi miwili.

 Ametoa maelekezo hayo jana alipofanya ziara ya kukagua nakufuatilia utekelezaji wa maagizo ya Serikali kuhusu kuondoa changamoto ya harufu na maji taka ya nayotirirka kupita mtaro unaopita kwenye makazi ya watu.

 Pia, ameelekeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Kanda yaKaskazini, wataalamu wa mazingira kutoka Ofisi za Mkuu wa Mkoa, Wilayana Halmashauri ya jiji la Arusha kufanya kazi kwapamoja kuhakikisha maeleekezo hayo yanatekelezwa.

 “Hamuwezi kujua hizi harufu mbaya za haya maji taka yanayotoka hapana kutiririka kwenye makazi ya watu zinaathari gani, sasaninatoamiezimiwilimkamilishemtambowahuu,”  alisema Mhe. Khamis.

 Aidha, naibu waziri huyo alisema kiwanda hicho kimekuwa kikilamikiwa na wanachi kwa muda mrefu kwa uchafuzi wa mazingira kwakutiririsha maji taka katika makazi ya wananchi.

 Hivyo, kutoka na nahali hiyo Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kwakutoa maeleekezo kwauongozi wa kiwanda kujenga mtambo wakusafishia maji taka kabla ya kwenda kwenye mazingira.

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi