Mchungaji wa Kanisa la Urejesho Nabii na Mtume Peter Nyaga amesema baada ya Mungu kumponya katika ugonjwa wa Corona ambao ulimfanya kulazwa ndani koma kwa siku kadhaa aliweza kupata ufunuo wa kuanzisha Tv itakayoweza kuoneshwa katika mataifa 72 ya Afrika , Ulaya na Marekani.
Akizizungumza wakati wa uzinduzi wa Tv hiyo ya Urejesho Tv yenye makao yake Makuu nchini Kenya, alisema alipokuwa nchini DRC Congo , alipokwenda kwaajili ya mahubiri February 2020, kuliibuka ugonjwa wa corona ambapo mipaka mingi ikafungwa.
Anasema alikaa kwa muda mrefu hivyo ilibidi kutumia lori la mafuta katika kurudi nyumbani, ambapo ilibidi ahudumie kama kondakta ili kuweza kufika nchini Tanzania.
Anasema katika safari yake hiyo aliweza kukutana na mikasa mingi, lakini alifanikiwa kufika salama Tanzania
Nyaga Anasema baada ya kuingia Tanzania aliweza kuugua ugonjwa wa Corona, uliompelekea kulazwa hadi baadhi ya watu na vyombo vya habari vikawa vinatangaza kwamba ameshafariki na kuzikwa na Manispaa.
Hata hivyo Mungu aliweza kumponya na kuruudi tena kwenye shughuli zake, ndipo akalikumbuka wazo lake la kufungua Tv ambayo itaweza kurusha Mahubiri kwa nchi zaidi ya 300 Duaniani.
Anasema hapo ndipo alipoanza mchakato wa kufungua kituo chake hicho, ambapo hadi sasa kinafanya kazi kwa nchi zaidi ya 72 zaidi ya nchi 30 zikiwa za Afrika.
Anasema kwa Tanzania kwa sasa anafunguo kituo cha kurushia matangazo hapa hapa, ambapo atakuwa akitoa ajira kwa waandishi wa habari , atapokea matangazo ya aina yote na kuendesha huduma zingine.
Kituo cha Mrejesho Tv amasema hakkitakuwa na ubaguzi wowote, kwa watu wa dini zote, vipindi vyote na matangazo kutoka kampuni yyoyote ambapo watapata nafasi ya kuonekana katika nchi za Afrika, Ulaya na Marekani.
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi