Alisema baada ya kupewa wazo hilo na kituo cha Voice Orphans Tanzania , aliamua kulibeba kwakuwa aliona ni jambo zuri akiwa kama diwani, na kuomba wakuu wa jeshi la polisi mikoani kote kutumia siku hiyo kwaajili ya kula na yatima.
"Tumemfukishia IGP Wambura na ametukubalia, na tutakula naye siku hiyo wakati kuonesha kwamba watoto yatima wapo mikononi salama katika mikono ya jeshi la polisi" alisema Rwakatale.
Mkurugenzi wa kituo hicho Maria Msaada alisema viongozi wote wa polisi katika mikoa yao watakuwa wanakula pamoja.
"Malengo ni kuonesha watoto yatima wapo salama mikononi mwa polisi, lakini pia kuwafanya watoto yatima wanapopata matatizo wawe wanakimbilia polisi" alisema.
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi