BAADA ya kuingia sokoni kwa filamu ya Hukumu Yangu,
mwigizaji Muksin Awadhi ‘Dr Cheni’ aamua
kumshirikisha Shabaki wa yanga Steven Mwamwala
na mchina maarufu aliyeshiriki katika shindano la Bongo Star Search.
Akizungumza
na Bongo Unit, alisema amewashirikisha katika filamu yake mpya, ambayo itaitwa Nimekubali Kuolewa, ambayo anaamini
italeta mabadiliko katika tasnia nzima.
Akimzungumiza shabiki wa Yanga, ambaye alipata umaarufu mkubwa kwa kulia baada ya timu ya Yanga
kufungwa 5 bila na Simba, ameona ni bora kumtumia ili kuongeza radha kwenye filamu yake hiyo.
“Najaribu
kuongeza radha ambayo watu wamekuwa wakiikosa, sio kila siku nije kitu kimoja
kile kile na waigizaji wale wale” alisema.
Filamu ya
Hukumu yangu imeingia sokoni, wiki hii baada ya kutangazwa sana na watu
kuisubiri kwa hamu.
Steven Mwamwala aliyelia baada ya yanga kufungwa na ya kufungwa 0-5 na Simba
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi