Kuvunjika kwa makundi mengi ya muziki, na
maigizo hupelekea baadhi ya malengo waliyopanga kuvunjika na kuwa kama ndoto.
Mkundi mbalimbali
ya sanaa yalianzishwa na kujipatia
umaarufu mkubwa, kama ilivyokuwa kwa
Fukoto, Kaole na mengine.
Hata
hivyo mwisho wake ni mpasuko mkubwa na
hata kufa kabisa kwa makundi hayo, na kushindwa kabisa kurudi na kufikia malengo waliyopanga
mwanzo.
Lakini tofauti sana kwa waigizaji Mrisho Zimbwa maarufu kama Tito Carlos na mwigizaji
mwenzake Pamela Brown ambaye sasa ni mkewe anayejulikana kwa jina la Shadya
Brown.
Walipoamua
kuungana kwaajili ya kufanya kazi pamoja ya filamu, na kujikuta katika vituko
na mikasa iliyopelekea hata kutaka kutoka roho ya mmoja wapo, na hatmaye
wanatimiza malengo kwa kukamilisha
filamu hiyo ingawa kulikuwa na kusuasua kwa muda mrefu.
Kukamilika
kwa filamu ya Kizazi ambayo mbayo mwanzo ilikuwa ikijulikana kama DNA, na
nilipoona baadhi ya scene na kugundua ni filamu nzuri na yenye kuvutia,
kulinifanya nifanye mahojiano Tito ambaye ndiye mwenye filamu.
Akizungumza
na mwandishi wa makala hii, Tito alisema tayari ameshaikamilisha filamu hiyo, ambayo inamuda wa zaidi ya miaka mitatu na miezi.
Alisema
kukamilika kwa filamu hiyo ni baada ya misuguano ya muda mrefu na kuamua kuyaweka matatizo yao pembeni.
“Tumepitia
misukosuko mingi ya maisha, lakini
tumeamua kuikamilisha na sasa inatarajia kuingia sokoni muda si mrefu,”
anasema.
Miongoni mwa
misukosuko ambayo ilitokea wakati wakiifanya filamu bado haijakamlika.
![]() |
| Tito akiwa na Bibi Hindu kwenye filamu ya Kizazi |
Kipindi filamu
hiyo inaanzwa kuigiza, Pamela alikuwa bize sana na kazi, hivyo akawa sehemu ya
uongozi wa filamu na sio mwigizaji.
Hata hivyo
baada ya filamu hiyo kuanza miezi kadhaa, ndipo patashika likaibuka baada ya
mwanamke kutokuwa na imani na mwigizaji wa kike aliyeigiza na mumewe.
Maelewano
yakawa hamna ukizingatia yeye pia ni kiongozi, maafikiano yaliyoamuliwa ni
kuondoa sehemu zote ‘Scene’ alizoigiza yule mwigizaji wa kike, ikawa sababu ya Pamela kuamua kuingia mwenyewe
na kushika nafasi hiyo.
Ingawa
alishika mwenyewe nafasi zote alizotaka kuigiza yule mwigizaji wa kike, vikaja
kuchanganyika na kazi ndipo akajikuta akikosa muda wa kuigiza na kupelekea
filamu kuendelea kubaki kimya.
Likaja tukio
lingine kubwa kiasi cha nusura kutoa roho ya mmoja wa wapenzi hao, pale mwaka
2011 baada ya Tito kupata ajali mbaya.
Tito anasema
baada ya matatizo ya muda mrefu na mpenzi wake kabla ya kuwa mkewe, kipindi
hicho akiwa mjamzito.
Ulitokea
ugonvi mkubwa, ambao alishindwa kuvumilia ndipo alipoamua kuondoka
nyumbani Magomeni, na kuelekea Bilicanas
kwaajili ya kupunguza mawazo.
Akiwa katika
klabu hiyo ya usiku pamoja na Ben Branco, anasema akili zake zilikuwa
zikimchanganya zaidi akaamua kujituliza
kwa kunywa pombe.
Anasema
ilipofika muda wa saa saba, ndipo walipoamua kubadili klabu na kutaka kwenda
Maisha Club.
Ilibidi
kutumia usafiri wa Pikipiki ambayo mara nyingi alikuwa akiutumia, ingawa
wenzake walimkataza lakini hakuweza kusikiliza hata kidogo.
Ilibidi
kufuatana na wenzake waliokuwa ndani ya gari, na yeye akiwafuata nyuma kwa
pikipiki.
Hapo
ukichanganya pombe, na mawazo mazito alipofika daraja la
Salender, akajikuta akiwaza zaidi juu ya mpenzi wake na hata kupelekea
kushindwa kulidhibiti pikpiki na kujikuta akipata ajali kubwa.
“Kosa kofia
ya pikipiki ilibidi nipasuke kichwa, lakini nilinusurika”
Katika ajali
hiyo, aliweza kuchubuka vibaya sana na hata kulazwa na baadaye kutolewa huku
akiwa bado anamatatizo ya kichwa.
Hapo ndipo
familia ilipokuja juu na kutaka aachane na huyo mwanamke, na mpango wa filamu
yao ya DNA ukawa umeishia hapo.
Ilichukua
miezi kadhaa kati ya Tito na Pamela kila mmoja akiamini hatoweza kurudiana na
mwenzake, lakini kila mmoja alijikuta wa wakati wake akijiraumu na kuungana
tena.
Kuungana kwa
mapenzi yao suala la kuiendeleza filamu ya DNA lilirudi tena na kuwa na imani,
ipo siku litaisha.
Katika tukio
lingine ambalo hawatakuja kulisahau baada ya kujifungua mtoto wao, ambaye pia
ni wa kwanza kwao anayeitwa Natalia.
“Lilikuwa
tatatizo jipya ndani ya familia, lakini likawa kubwa sana kiasi cha kufikishana
mahakamani” anasema.
Wivu wa
mapenzi ulizidi kutawala, kiasi cha kipigo kuwa sehemu ya maisha yao na hata
kutokuwa na maelewano hadi kufikishana mahakamani.
Mwaka 2012
baada ya kufungua kesi na ndipo mambo yalipovunjika tena, na kusitisha filamu
ya DNA na ndipo Tito aliamua kutaka kutoa Scene zote zlizomweka mkewe na
kumweka mtu mwingine.
Lakini
ukubwa wa ghalama ulimfanya asubiri, huku akiudhulia mahakamani baada ya
kufikishwa na mkewe.
Hata hivyo
wakati kesi yao ikiendelea mlalamikaji akiwa Pamela na familia yake, juu ya
Tito mambo yalikuwa tofauti kwa wao.
Kesi
iliendelea na wakati huo wakijisurisha wenyewe nyumbani, hadi mwisho wa siku
wakawa wanatoka katika chumba kimoja kwenda kwenye kesi, jambo ambalo
liliangusha mshangao mkubwa kwa watu wanaowajua.
Kweli
mapenzi ya watu usiyaingilie, leo hii Tito anasema tayari wameshamaliza
migogoro yao yote na wameshakamilisha filamu ya DNA, ambayo wameamua kuipa jina
la KIZAZI.
“Filamu muda
wowote inaweza kuingia sokoni, na tumeona haina haja ya kuendelea kurumbana na
kupoteza fedha nyingi”
Tito jina
lake harisi ni Mrisho Salehe Zimbwe akiwa ni mtoto wa 5, mzaliwa wa Tanga pia
ni baba wa watoto watatu, Amina, Abdulimajid na Natalia.
Baada ya
kuingia jijini Dar es salaam, akajiunga na kundi la sanaa la Kaole, mwaka 2002 na kuwa miongoni mwa wasanii wa mwanzo wa
kundi hilo.
Filamu yake
ya kwanza kuigiza ni Chumba no 77 ambazo zilikuwa filamu za mwanzo, na kuleta
mapinduzi makubwa hadi sasa.
Filamu
ambazo amekuwa akifanya vizuri sana ni zile za mapambano, kwakuwa watu aliokuwa
akifuata nyayo zao ni Jimmy Master na Kaini.
Mwisho



No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi