Baada ya kuangaika kwa muda mrefu katika
tasnia ya filamu kwa kucheza filamu za watu, mwigizaji Yobnesh Yusuph ‘Batuli’
ameamua kueleza juu ya mikakati yake mpya katika filamu baada ya kupata meneja
wa kumwezesha katika kazi hizo.
Akizungumzia
ndoto zake nyota huyo, ambaye alishawahi kufanya kazi nzuri katika filamu
ya Fungate, Glory of Ramadhani, Waves of Sorrow huku akishirikiana na wasanii
Kama Steve Mangele ‘Steve Nyerere’ Vicent Kigosi ‘Ray’, marehemu Steven
Kanumba, Issa Mussa ‘Cloud 112’ na wasanii wengine kibao ambao ameshafanya nao
kazi.
Batuli
anasema kwa muda mrefu alikuwa akitumikia filamu za watu, ili kujiweka katika
nafasi nzuri ya kutambuliwa na kujilikana zaidi.
Lakini
anasema kikubwa alikuwa bado alikuwa hajakamilika katika kufanya kazi zake
mwenyewe hususani katika upande wa bajeti, kwakuwa hakutaka kufanya kazi
zilizopoa na kudorola.
Kwa sasa
nyota huyo ambaye anaumaarufu mkubwa, anasema amejipanga kuachia filamu zake
tatu tofauti, ambazo pia ni filamu zake
za mwanzo chini ya uongozi wake mpya.
Anasema
tangu alipoingia mkataba na meneja huyo mpya, zaidi ya miezi miwili iliyopita
hivi sasa tayari ameshaanza kuandaa filamu tatu mfuririzo pamoja na matangazo
ya Tv.
Batuli
anasema filamu yake ya kwanza inaitwa Wekeza Inalipa, ambayo pia ameifanyia
kipindi katika moja ya stesheni za Tv ili kuhamasisha watu kuwekeza hasa katika
hisa.
“Katika
filamu hiyo huwa nazungumzia umuhimu wa watu wa kununua hisa, ni moja ya filamu
zangu za tofauti sana na nzuri kwa mimi naikubali sana,” anasema.
Filamu hiyo
anasema imeambatana na matukio ya mbalimbali ya kutoa elimu na kuwafunza watu waweze kujali zaidi maisha ya
baadaye, hasa kwa kununua hisa ambazo zinaweza kusaidia maisha yao kwa
kupambana na umaskini.
Zaidi ya
filamu anasema pia amefanya kipindi akiwa kama mtangazaji, katika moja ya stesheni
ambazo zitakuwa zikionyesha tangazo hilo la Wekeza Inalipa.
Filamu yake
ya pili anasema kwa sasa ndiyo ipo kwenye mikakati ya mwisho katika
uchanganyaji wa picha ‘Editing’, ambao ameshirikiana na wasanii kutoka Afrika
mashariki na kati.
“Kwa sasa
bado sijaruhusiwa kuwataja wala kutaja jina la filamu kwakuwa bado tupo kwenye
mkakati wa kuahkikisha inaisha na kuitangaza kabla ya kuingia sokoni” anasema.
Anasema kazi
hizo zote zinampa moyo juu ya matarajio yake ya kuwa miongoni mwa wasanii
wakubwa wa Afrika mashariki na kati na Afrika nzima, katika suala zima la
filamu.
“Tunaelekea
vizuri katika kazi nzuri ya filamu, ambao itawezesha wasanii kufika mbali
hususani kutokana na malengo yetu” anaendelea kusema.
Batuli
anasema hivyo amejipanga amejipanga zaidi kufanya filamu zenye stori nzuri na
zenye mvuto, kuanzia mavazi hadi waigizaji ili kupamba na soko la kimataifa
kuliko kuangalia zaidi soko la ndani.
Kuhusu kuwa
na meneja anasema maamuzi yake ya kutafuta meneja kwaajili ya kazi yake, si
kwamba alikurupuka kuwa na meneja
ilimradi meneja.
Isipokuwa
alifikiria na kuamua kutafuta meneja ambaye anawez kusimamia kazi yake, na
kumfikisha katika kiwango cha kimataifa zaidi.
Anasema
wasanii wengi wamekuwa wakiangaika wenyewe bila ya kuwa na uongozi, au meneja atakayeweza
kusimamia vizuri kazi zake, kwa tena kwa sheria za nchi.
“Anasema
wasanii wengi wamekuwa hawana elimu ya
kutosha, kuhusiana na usimamizi wa kazi
zao, na ndio maana wamekuwa wakiburutwa bila ya kujua washike wapi” anasema.
Hivyo kwa
msanii kuwa na meneja kutamsaidi baadhi
ya kazi zake za sanaa kuwa chini ya usimamizi mzuri, bila ya msanii kuathirika na chochote.
Anasema mara
nyingi wasanii wengine wanatafuta mameneja ambaye, hawezi kumsaidia isipokuwa
meneja ndiyo anamtegemea msanii.
Batuli
anasema meneja ni lazima aijue biashara
ambayo anaenda kuiwekeza, na kujua
hasara na faida ya kazi yake.
Kufanya
hivyo kutamwezesha kuweza kufika mbali, kwa msanii na meneja mwenyewe.
“Kama
ninakuwa na wazo la simulizi ya filamu,
huwa nalifikisha kwa meneja wangu, ambaye naye anakuwa na watu wake kwa pamoja
wanaiangalia na kuniambia na baadaye kufanya kazi baada ya kuona inafaa” anafafanua
zaidi.
Anasema hiyo
ndiyo kazi kubwa ya meneja wake na kama kuna lingine basi huwa wanakaa chini na
kujadiliana, ili kufika mwafaka.
Kwa sasa
Batuli anasema lengo lake ni kufika katika anga za filamu za kimataifa za zenye kiwango cha juu,
ikiwemo kuwashirikisha waigizaji kutoka
na wenye uwezo mkubwa wa kuigiza.
Kwa muda wa
miezi miwili, anasema tangu aingie
mkataba na meneja huyo, anasema tayari ameshaanza kuona mafanikio makubwa
ambayo anaamini, yatamwezesha kufika mbali zaidi.
Nyota huyo
pia amesema hapendizwi na wasanii wanaovaa nguo za fupi na zenye kuonesha
sehemu ya mauongo yao.
Anasema
kuvaa za namna hiyo, sio kwamba wanaweza
kusaidi kazi zao kuuzika, ila wanajidhalilisha kutokana na Watanzania sasa
wamebadilika na wanaangalia kazi zaidi.
Anaendelea
kusema kwamba ingawa ni maarufu, lakini
hajalewa na sifa na ndiyo maana ameamua kujikita zaidi katika filamu za kiwango
cha juu.
“Siku hizi
watu hawaangali unavaaje? au mzuri kwa kiasi gani isipokuwa wanaangalia kazi
yako ipo vipi” anasema.
Batuli
anasema kwa sasa nguvu zake zote amaeamua kuwekeza kwenye kazi zake mpya, ili
kuweza kufanikiwa na kujenga jina kubwa.
Batuli
anasema yeye ni mama wa mtoto mmoja, alianza kuigiza mwaka 2008 katika filamu
ya Mkasa.
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi