Suala la uigizaji
kwa nchi za wenzetu ni kitu ambacho kinahitaji umakini zaidi, maana unaweza
kusababisha madhara makubwa au kupoteza uhai wa mtu.
Hii
ilijitokeza katika baadhi ya filamu, kama Cyborg ya Jean Cloud Van Damme
alipomtoboa mtu jicho katika harakati za kuigiza.
Au San Datty
alipoua kwa bahati mbaya wakati akiigiza, kwahiyo yoyote yanaweza kutokea,
ingawa kwetu ni tofauti sana kwakuwa watu wanaigiza zaidi kuliko uhalisi wa
kitu wanachokiigizia.
Lakini
tofauti na filamu ya The Gal Gradder, ambayo imechezwa Kenya na mwi[gizaji Baby
Joseph Madaha ambaye pia alikuwa mshiriki wa tamasha la Bongo Star Search, pale
aliponusurika kuua, kuuwawa na hata kubakwa.
Akizungumza
na mwandishi wa makala hii, alisema ni tofauti sana na uigizaji wa kitanzania,
kwani amegundua mara nyingi unapotafuta uharisi wa jambo basi tegemea matukio
ya hatari kujitokeza.
Alisema
wakati akiigiza filamu hiyo, ambayo inatarajia kutoka mwezi huu Desemba,
alikutana na mambo mengi ambayo mengine yalifanya maisha yake kuwa hatiani.
“Nikiwa
nyumbani Tanzania nimeigiza filamu nyingi, lakini sikuwahi kuona na naingia
matatizoni kama ilivyokuwa kwa filamu hii” anasema
Alielezea
zaidi kwamba filamu hiyo, ilikuwa ikihusu juu ya matukio ya vijana waishio
mitaani, kwa nchini Kenya wanajulikana zaidi kwa jina la Chokoraa.
Vijana ambao
wamekubwa na mikasa mingi, amba;yo hatmaye wamejikuta wakiwa na roho ya kijana
na kufanya mauaji mengi.
Anasema
kutokana na kisa hicho, ikabidi filamu hiyo iigize sehemu harisi ya matukio
hayo, kwa kuwa tayari walishafanya uchunguzi na kugundua ni sehemu gani zaidi
ambazo inaweza kuwa harisi.
Kwakuwa
meneja wa kampuni ya Candy n Candy, Joe na ndiye mmiliki wa filamu hiyo, ni mtu
wa Kenya, hawakuwa na wasi wasi juu ya usalama wao.
Anasema
tukio la kwanza ambalo liliwakumba, walienda kuigiza kwenye majumba ambayo
watoto wa mtaani ambao wanakuwa wakiishi mara kwa mara.
Lakini kumbe
wakati wakiigiza katika eneo moja la mtaa, kwa upande wa pili wa mtaa huo huo
yanatokea mauaji ya kweli, ya mtu raia wa Kichina.
Anasema
mauaji hayo yaliwafanya wasitishe tukio la kuigiza kwa muda furani, kwakuwa wao
walikuja kuyashitukia wakati tayari yameshatokea.
“Chokoraa wa
Kenya au majambazi wa huko, kila kitu wanafanya kimya kimya. Unaweza ukawa nje
na ndani watu wakawa wanafanya unyama bila yaw ewe kujua.” Alielezea Madaha.
Baada ya
kuisha kumbukumbu ya tukio hilo anasema likaja tukio lingine, ambalo alikusa
watoto wa Kenya ambao ilipaswa waigize kama watoto wa mtaani ambao pia ni
waharifu.
Kwa kuwa
Madaha, aliigiza kama kiongozi wa watoto wa mtaani, ilibidi waigie katika
makazi ya Chokoraa wa ukweli ili wapate kuigiza kipande hicho.
Anasema
ilibidi yeye aonekane kama vile anatoa amri kwa watoto hao, waingie mtaani na
kuvamia watu na baadaye kumletea kile ambacho wamekipata.
Lakini bila
kujua kama makazi waliyoingia chokoraa wa kweli walikuwepo, ambao ndiyo sehemu
zao za kujificha wanapofanya uharifu.
Kitendo cha
wao kuingia eneo hilo, walijikuta ghafla wamevamiwa na Chokoraa hao wa kweli,
wakiwa wameshika sirahaa kama mapanga na vitu vingine.
“Bosi wangu
Jor, alikuwa na dola mia nane zote walichukua. Mimi nikapigwa sana, hadi
nikavimba jicho.
Wakati huo
kameraman, alikuwa amekimbia na kujificha kwenye mtalo ili kuhofia kuchukuliwa
kamera yake,” anaelezea kwamba.
Wale watoto
ambao wao walikuwa wakiigiza kama chokoraa, nao walikula kipigo cha nguvu kiasi
cha kukimbia kila mmoja na njia yake.
“Ilikuwa
nusura sana kwani kipigo tulichopigwa kilikuwa kikubwa. Nashukuru mungu
hawajatufanyia uharifu mwingine maana wangeweza hata kutuchoma kisu” anasema.
Baada ya
tukio hilo anasema tukio lingine ambalo nalo lilikuwa hatari wakati wanaigiza
filamu hiyo, lilikuwa la kuigiza akimgonga mtu.
Tukio hilo
lilimpasa yule ambaye anaigiza akigongwa, ilimbidi alirukie gari wakati
linapokuja, jambo ambalo walifanikiwa kufanya hivyo kwa mra ya kwanza.
Lakini tukio
hilo lilibidi lirudiwe kwa mra ya pili, ndipo balaa lilipoibuka, “Kwa mara ya
pili, nilikanyaga mafuta na kumfuata yule mtu. Lakini sijui ibirisi gani
alinipitia mbele yake, kwani gari ghafra
breki ziligoma.
Na yule mtu
bila kujua kama breki ziligoma alizidi kusimama bele na alipolirukia, alijikuta
nikimgonga kweli,” anasema.
Hakuna
aliyeamini kama angepona, kwani alirushwa hadi mtaloni na kuzimia papo hapo,
hali iliyobidi wamkimbizie hospitali kwaajili ya huduma za kwa nza.
“Hadi leo
ukienda kwa Kenya, na kuwaambia watu waigize na mimi nishike kisu au ajali,
wanakataa wanajua sina masihara” anasema Mahada.
Lakini
anasema siku moja kulikuwa na tukio lingie ambalo lilibidi waigiz kama vile
anashikwa makalio na wateja wa baa, lakini baadaye wanamvuta chooni na kumbaka
kwa nguvu
Lakini
anasema kabla ya kuigiza tukio hilo, ilibidi wapumzike baada ya kazi
zinginekuisha.
Lakini
wakati wakipumzika wale waliokuwa wakiigiza kumbaka, ilibidi waanze kunywa zile
pombe za kuigia.
Hadi muda wa
kuigiza ulipofika walikuwa tayari walishalewa kweli, lakini watu hawakujua kama
walikuwa wamelewa sana.
“Nilikuwa
naigiza kama muhudumu, na kuwaletea vinywaji.
Ndipo nikashikwa makalio, lakini kushikwa kwake ilikuwa tofauti na kule
kuigiza. Nilishituka lakini nikanyamaza, lakini kasheshe ikaja pale katika
kubaka ndipo hali ilipobadilika ghafla.” Anaendelea kusema.
Waigizaji
hao ambao raia wa Kikenya, walianza kumgombania kwa nguvu, na ndipo hapo Baby
alipojikuta akipoteza nguvu za kweli, maana vidume vya watu walikuwa na uroho
wa kweli.
Waliokuwa
wakiangalia walijua kazi inaenda vizuri, lakini wakaja kushituka aada ya kuona
nguo zikianza kuchanwa, huku watu wakiwa na lengo la kubaka kweli.
“Walijitahidi
kusimamishwa lakini, walikuwa bado wamepania kunibaka kweli. Ndipo watu
wakaamua kuingilia kati na kuanza kuamulia ili kunitoa,” aliendelea kusimulia
mkasa huo kwa kusema.
Baada ya
kutolewa ndipo nguo zao zilipoonyesha lengo lao, na hata kusimama vizuri
walishindwa kwani walikuwa wakinesa sana.
Lakini tukio
la mwisho lilikuwa pale alipotekwa na mtu ambaye alimfanyia unyama, ilimbidi
mtu huyo amtese kwa kumtumbukiza kwenye maji.
“Ilibidi
anitumbukize kwenye maji mara moja, lakini hatmaye alinikandamizi moja kwa moja
na hatmaye nikaanza kupoteza punzi na kunywa maji.
Watu
walikuwa wakiangalia kupitia Tv, ndogo ambayo ilikuwa ndani ya maji ndio
waliweza kushituka baada ya kuniona natapatapa.” Anasema
Ndipo
walipomwambia wamchie, na baada ya kuachiwa hapo alianguka chini kama mzigo na
ndipo walipogundua alikuwa hoi, maji yameingia puani na mdomoni.
Hayo ni
baadhi ya matukio makubwa yaliyomkuta Baby Madaha, kwenye filamu hiyo ya The
Gal Gladder.
Hata hivyo
anasema filamu hiyo anaamini itaendelea kuwa kumbukumbu kwa maisha yake, kutokana na mikasa mikubwa iliyomkuta.
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi