| (Meneja Chizo Mapesa) |
Meneja wa
mwanamuziki huyo ambaye anaitwa Ally
Amiri ‘Chizo Mapesa’ alisema amejipanga kumtangaza na kumuongoza kutokana na kazi zake. Aidha meneja
huyo ambaye pia likuwa meneja wa mwanzo wa mwanamuziki Naseeb Abdul ‘Diamond
Plutnum’, alisema kwa muda mrefu aliacha kudhamini wasanii baada ya mara ya
mwisho kuachana na mwanamuziki huyo.
Anasema kwa
mara ya kwanza alimukuta nyota huyo ambaye kwa sasa anatamba na kibao cha Kesho
na Nataka kulewa, akiwa na wimbo mmoja
wa Toka Mwanzo.
Anasema
aliamua kuingia naye mkataba kwa muda wa miaka mitatu, na kwaajili ya
kusimamamia kazi zake zote, ikiwemo chakula na mavazi.
kazi zake za
muziki, na tulifanya makubaliana hayo kwa mjumbe wa mtaaa wa Kongo Kariakoo” alisisitiza
meneja wa zamani wa Diamond ambaye ni wasasa wa Mau G.
Baada ya
kusainiwa mkataba kuanzia mwaka 2007 hadi 2010, ndipo nikasimamia kazi hiyo ya
kwanza kuanzia matangazo, video na mavazi.
Anasema
baada ya hapo ndipo wakaanza kwenda mbio katika kukamilisha kazi zingine,
ambapo alitengeneza wimbo kama G Sachi, Wa kunesanesa na Si upo tayari ambayo
yote mwaka 2008.
“Baada ya
hapo niliibiwa vitu vyangu katika ofisi yangu na kuibiwa kila kitu” alifafanua.
Meneja
anasema baada ya kuibiwa vitu vyake aliishia kabisa fedha, na ndipo msanii huyo
alipoamua kuondoka na siku chache baadaye ilitoka wimbo wa Kamwambie.
Chizo Mapene
amesema hivi sasa ameamua kurudi tena kwenye tasnia hiyo kwa kumdhamini kaka
yake, ambaye kwa sasa naye amaamua kujikita kwenye muziki huo.
“Nimeamua
kurudi tena kwa lengo la kufan ya kazi iliyokuwa bora na mtu ambaye namtegemea
na kazi zake nimekuwa nikizipenda” alisema.
Na Huyu ndio Mau G ambaye anakuja kufanya makali, kupitia meneja Chizo Mapesa
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi