Baada ya
kutamba na wimbo wa Naomba Kidogo , Mwanamuziki Hasnat Conner ‘Hasnat’ ameombwa
kupeleka nyimbo tano katika kituo cha televisheni cha Afrika Kusini Channel O.
Aliimbia Bongo Unit mwanamuziki huyo, ambaye hivi sasa yupo katika kundi la Kazi Kwanza baadaya kuuzwa katika kundi la Mkubwa na
Wanawe alisema tayari ameshapeleka nyimbo zote tano siku ya juzi.
Alisema
ingawa alikuwa amehama kundi hilo, lakini kazi nzima ya kutengeneza na kupeleka
nyimbo hizo zimefanywa chini ya uongozi wa mkubwa na wanawe iliyo chini ya
Saidi Fella.
“Kazi tayari
nimeshapeleka nachosubiri kusikilizia kama kuna lingine litahitajika, kwani
yote namsikiliza Fella” alisema.
Nyimbo
ambazo alizitunga na kuzituma ni Sina
Shaka,Mitungi,Naomba Kigogo,Nakunaku na Mapozi.

No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi