MSANII nyota wa uchekeshaji hapa
nchini, Hussein Mkiete, maarufu kama 'Sharomilionea' anatarajia kuzikwa kesho
(Jumatano) huko kijijini kwao Lusanga, Lushoto mkoani Tanga.
Kifo cha mchekeshaji huyo kimegusa
hisia za walio wengi, ambapo msanii mwenzake King Majuto alikimbizwa Hospitali baada ya
kushikwa na presha, ambayo ilihatarisha maisha yake pia.
Kwa mujibu wa mtoto wa King Majuto,
Hamza Majuto, hali ya baba yake
inaendelea vizuri kutokana na kuumizwa zaidi na msiba wa Sharomlionea
anayetamba katika ulingo wa filamu na muziki hapa nchini.
Msanii huyo alikufa
jana saa mbili za usiku Maguzoni, kilimita chache na kijijini kwao Lusanga,
wilayani Muheza mkoani Tanga, baada ya gari lake alilokuwa akisafiria lenye
namba za usajili T478 BVR Toyota Harrier kupinduka na kusababisha kifo chake.
Taarifa za kifo hicho zilithibitishwa
na Kamanda wa Polisi mkoani Tanga, Constantine Masawe, na kusema kuwa mwili
wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Teule, Muheza, mkoani Tanga kwa taratibu
za mazishi zinazopangwa na familia yake.

Sharomilionea ameshacheza filamu nyingi
za uchekeshaji na kujipatia sifa kubwa, ikiwamo ile ya Sharo Millionea, Imekula
Kwako, Jini Mahaba, Porojo na nyinginezo zinazofanya vyema katika tasnia ya
filamu nchini.
Wasanii wengi wa tasnia ya filamu na
muziki waliozungumzia kifo cha Sharomillionea wakiongozwa na Steve Nyerere, wameonyesha
kuchanganyikiwa kwa msiba wa msanii huyo.
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi