Baada ya kuwa kwenye
rotation kali na video ya Fid Q, "sihitaji Marafiki", mwimbaji Yvonne
Mwale anatoa video mpya. Wimbo unaitwa "Familia Yangu" ambayo ni single
yake ya pili kutoka kwenye albamu yake inayoitwa "Kalamatila". Album
hiyo imerekodiwa chini ya Caravan Records na tayari ipo sokooni.
Inapatikani kwenye maduka ya vitabu "A Novel Idea", pamoja na iTunes.
Yvonne MwaleTitle: Familia YanguAlbum: Kalamatila (2012)Label: Caravan RecordsDirector: Matthias Krämer
"Familia
Yangu" ni wimbo wa kwanza katika lugha ya kiswahili kutoka kwa Yvonne
Mwale ambayo ametoka Zambia. Anasema: "Kwenye album yangu "Kalamatila"
nimeimba nyimbo za lugha za nyumbani na kingerezi, ila nilipata wito wa
kuimba katika lugha ya kiswahili baada ya kuhamia nchini Tanzania".
Track hiyo inazungumzia changamoto inayo tokana na matatizo ya fedha
kati ya mke na mume wake.......
Ingawa
ni muda mfupi imepita tangu Yvone Mwale alizindua album yake ya
"Kalamatila", mwimbaji huyu siyo chipukizi, bali ni msanii wa muda mrefu
mwenye mafanikio mbali mbali katika game la mziki. Mwaka 2009 alishinda
tuzo ya "Msani Bora wa Upcoming" Kwenye Zambia Music Awards. Baada ya
kupata tuzo hilo alishinda tuzo ya Music Cross Roads (Afrika nzima) na
bendi yaki Nyali Band na akaendelea kufanya tour nchi tisa Ulaya.
Alivorudi alipata nafasi ya kupaform na Oliver Mtukudzi Malawi kwenye
Tamasha inayoitwa "Lake of Stars".
Baada
ya kufika Tanzania alipata nafasi kupaform na wasani mbali mbali
wakiwemo, Mzungu Kichaa na Fid Q na wasanii wakimataifa kama, Maya
Azucena, Bobby Rickets na Dobet Gnahoré. Mwezi uliyopita alishinda
nafasi ya pili katika shindano la Mziki - Jahazi Jazz Music Competition.
Hivi
sasa, Yvonne Mwale anarekodi na wasanii mbali mbali kutoka bara la
Afrika na management yako wana andaa show kadhaa mwishoni mwa mwaka huu.

No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi