Angalia picha zake zaidi akiwa kwenye pozi
Thursday, September 27, 2012
Mjue mwigizaji wa kike anayetikisa kwa sasa
Katika kuibuka kwa wasanii wapya wa kike na pia kupotea kwa baadhi yao leo hii blog yako ya BONGO UNIT, ambayo haina mbwembwe sana ila zaidi ni kukuletea utamu unaohusu wasanii wetu wa humu humu ndani, ili kuweza kuinua tasnia yetu. Leo hii nawaleteni msanii ambaye kwa sasa ndiye anayekuja kwa kasi na kuchukua nafasi za wasanii wengine ambao walikuwa wakivuma na sasa kupotea taratibu. Jina halisi ni Yobnesh Yusuph aambalo anapenda kulitumia kisanii ni Batuli . Mwigizaji huyu anasifa za urefu ana mwili mnene kiasi, ngozi wanasema maji ya kunde, mcheshi na asiyejua kukasirika hadi sasa ameshaigiza filamu zaidi ya tano zilizotoka, ikiwemo Glory to Ramadhan ya Vicent Kigosi 'Ray' wa kampuni ya Rj , na ambazo ameigiza ila bado hazijaingia sokoni ni nyingi ikiwemo Long Time, Get Out za Stive Nyerere kutoka kampuni ya Nyerere The Power, Waves of Sorrow ya Vicent Kigosi, Fungate ya Cloud 112 katika kampuni yake ya CY & CY na Cost To Cost ya Slim. Hebu pata picha zake na uone kazi zake
Angalia picha zake zaidi akiwa kwenye pozi
Angalia picha zake zaidi akiwa kwenye pozi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi