Wednesday, September 26, 2012

Kanumba aendelea kupigwa Changa la Macho

Mkurugenzi na kampuni ya ASET inayomiliki bendi ya Twanga Pepeta, ameilalamikia kampuni PAPA-ZI, ambayo imekaa na albamu ya wimbo wa marehemu Steven Kanumba kwa muda wote akiwa hai hadi sasa amefariki dunia.Asha Baraka anasema kwamba marehemu Kanumba alichukuliwa na Urban Pulse chini yake,  kwaajili ya kwenda kuigiza filamu ya Lovely Gamble, na baadaye wakampenda kutokana na kipaji chake cha kuimba, jambo ambalo wakafikiria kutengeneza  albamu ya wimbo akiwa huko huko Ulaya, baada ya marehemu kuonyesha mistari yake.
Asha anaelezea  baada kufanya filamu hiyo ndipo wakaingia studio kwaajili ya kufanya kazi ya nyimbombalimbali  moja wapo ni ile  iliyokuwa  ikitabiri kifo chake. Anaendelea kueleza  kwamba, baada ya kurudi nchini, akiwa na Mahojiano mbalimbali ya Marehemu Kanumba, akiwa Ulaya, walitarajia(Soma zaidi ujue kichijiri)
kuyetengenezea Cd moja na kuuza, pia albamu yake ya nyimbo kuitengeneza na kuuza ikiwa kama albamu ya muziki. Asha anazidi kuelezea baada ya kuwapa PAPA-ZI albmu hiyo kwaajili ya kuisambaza lakini cha kushangaza kwamba wamekaa nayo kwa muda mrefu hadi sasa bila ya kuitoa wala kuisambaza.
Anasema mpaka filamu ya Lovely Gamble inaingia sokoni, hadi Kanumba anapatwa na umauti lakini bado wameendelea kuing'ang'ania, bila majibu yoyote.
 Mkurugenzi huo aliendelea kusema baada ya Kanumba kufariki, walitoa fedha za Kitanzania Milioni tatu, ambazo yeye aliamua kuzifikisha kwenye msiba kwa familia yake.
   Asha anasema baada ya hapo zimeendelea kuwa stori, pindi akiwapigia simu wanamzungusha, kwakuwa yeye ndiyo aliingia mkataba juu ya umiliki wa kazi hiyo, hivyo jambo ambalo wanampa wakati mgumu kwani hajalipa fedha ambazo alizifanyia kazi hiyo.
    Asha aliendelea kusema imefikia kiasi cha kushindwa kusafiri kwenda Ulaya kwa kuhofia deni kubwa alilonalona majibu ya kutosha juu ya albamu hiyo, kwani alitegemea ingeuzwa na kuwalipa wale walioifanya hiyokazi.

Mwisho Asha Baraka aliwaomba uongozi wa kampuni hiyo,kumrudishia kazi yake ili akasambaze sehemu nyingine, kwakuwa Steps Entertaiment imekubali kuisambaza, kwakuwa wao wamekuwa wasambazaji wa msanii huyo kwa kila kazi yake kwa muda mrefu.

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi