|
Taarifa kutoka kwenye meli Seagul
ambayo inasadikiwa imebeba abiria takriban 280 imezama katika Bahari ya Hindi eneo la Chumbe kisiwani Zanzibar inasema
kwamba watu takribani 60 wamekufa kwenye ajali hiyo. Meli hiyo ambayo inatumia jina SKAGIT ilikuwa inatoka Dar Es Salam
kuelekea Zanzibar, kwa taarifa
kutoka kwa vikosi vya wanamaji , inasema kwamba meli hiyo
ilianza kupata matatizo baada ya kutokea mawimbi makali. Hata hivyo Jeshi la polisi la
wanamaji nchini Tanzania limeanza shughuli za kuwaokoa watu zaidi ya mbia mbili
wanaohofiwa kuwa kwenye meli ya Skagit inayoripotiwa kuzama huko visiwani
Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa za polisi,
ingawa hawajathibitisha idadi kamili ya abiria waliomo kwenye meli hiyo, lakini
wamethibitisha kwamba meli hiyo imepigwa na dharuba ya upepo mkali katika eneo
la Chumbe pindi ilipokuwa inatoka jijini Dar es Salaam kuelekea visiwani
Zanzibar.
Itakumbukwa kwamba, ni takriban
mwaka mmoja sasa tokea ajali ya meli iliyokuwa imezidisha mizigo kuzama katika
pwani ya kisiwa cha Zanzibar ikiwa na watu takriban 800.
|
No comments:
Post a Comment
https://www.facebook.com/gomesamohamedi