Saturday, July 14, 2012

Wasanii waanza vikao vya harusi ya William Mtitu


Mwigizaji wa filamu nchini William Mtitu yupo kwenye mikakati ya kufunga ndoa Septembe 8mwaka huu. Vikao vimeshaanza katika kurekebisha mambo ya harusi yake, ambayo mwenyekiti wa kikao cha harusi yake ni Jacob Stephan 'Jb'. William Mtitu amesema mwanamke anayetaka kumuoa ni yule yule mpenzi wake wa muda mrefu, ambaye hausiki katika masuala ya sanaa ya filamu. Pia wasanii hao wapo katika mikakati ya kujua harusi hiyo itaenda vipi, Mc atoke wapi na ukumbi maeneo gani na jinsi ya kuendesha shughuli nzima. Hata hivyo kikao hicho bado hakijaenda sawa, kwakuwa leo wasanii wengine wamegawanyika wengine wameenda ZIFF, na wengine wapo IRINGA, wakati Mtitu yupo Shooting.

Steve Nyerere aliyevaa mawani akiwa amepozi, Vicent kigosi pembeni, wakati Cloud 112 akiwa amesimama pamoja na Haji Adam 'Baba Haji'.

Rachal akiwa na mama Loraa
Kulia ni Irene Uwoya, akiwa pamoja na bibi harusi mtarajiwa Ant Ezekiel pamoja na Snura

Cloud akisikiliza kwa umakini.

Baba Haji akitoa hoja mabyo ilikuwa ikipigwa na Cloud juu ya Mc awe msanii au awe nje ya msanii.

Jb akitoa maoni yake kwamba Mc akiwa msanii faida gani watapata

Haji Adam pamoja na Ant Ezekiel

Mtitu akisikiliza kwa umakini jinsi kikao kinavyo kwenda

Jb pembeni yake ni Uwoya

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi