Friday, July 6, 2012

Epiq Bongo Star Search yazidikupaa


Video zilizochukuliwa leo kwenye banda la Zantel Saba Saba ambapo Majaji wa EBSS walipata nafasi ya kutembelea kujionea maonyesho yanaondelea ikiwa  ni pamoja na kukutana na waandishi wa habari kuelezea waliyoshuhudia katika usaili wa mikoa mitatu waliyopitia ya Dodoma , Zanzibar na Lindi . Pia waliweza kutoa sifa wanazoziangalia katika kutafuta vipaji vya muziki pamoja na kueleza eneo la usahili unaofuata wiki hii plae mjini Arusha sehemu inayoitwa Triple A.  
Pamoja na hayo, Mkuu wa Masoko kutoka Zantel bwana . Deepak K. Gupta na Mkuu wa mawasiliano Awaichi Mawalla walipata nafasi ya kuelezea njia mpya ambayo wenye vipaji vya kuimba lakini wakakosa nafasi ya kufanya usaili wanaweza kufanya usaili kupitia simu zao za mkononi. Mfumo huu ni wa sauti ambapo mshiriki anapewa nafasi ya kuimba nyimbo aitakayo kwa muda usiiozidi dakika moja na kuweza kupata nafasi ya kusikilizwa na Majaji.







Vicky akielezea kidogo

No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi