Thursday, June 14, 2012

Vitabaridi yatikisa sokoni

Baada ya  filamu za DJ Ben na Taxi Driver zikiendelea kuwa gumzo, mkongwe Steven Jacob `JB’ anayemiliki kampuni ya utengenezaji filamu ya Jerusalem anakusudia kuibuka na filamu mpya, Vita Baridi itakayoshirikisha mastaa wa nchi nne tofauti.

Ameiambia safu hii kuwa, kwake itakuwa filamu ya kwanza kukutanisha wasanii wakali kutoka katika nchi tofauti na inayozungumzia mapenzi kwa namna tofauti.

“Ni filamu ambayo imeigizwa na kuzungumzia mapenzi katika mtindo ambao hakuna  mtu angefikiria kama upo namna hiyo,” alisema JB aliyewataja wasanii walioshirikishwa ni Cassie Kabwita wa Zambia, Patcho Mwamba wa Demokrasia ya  Kongo ambaye anafanya kazi ya muziki nchini, Makombora wa Zanzibar, JB mwenyewe na Kajala wanatoka Tanzania Bara.


No comments:

Post a Comment

https://www.facebook.com/gomesamohamedi